Fahamu ufafanuzi wa kipimo cha Hepatitis B Surface Antigen (HbsAg)
Kipimo cha homa ya ini aina ya Hepatitis B Surface Antigen, ni kipimo cha kwanza kumtambua mtu kama ameambukizwa virus vya homa ya ini aina B
𝗛𝗘𝗣𝗔𝗧𝗜𝗧𝗜𝗦 𝗕 𝗦𝗨𝗥𝗙𝗔𝗖𝗘 𝗔𝗡𝗧𝗜𝗚𝗘𝗡 𝗡𝗜 𝗡𝗜𝗡𝗜?
Hepatitis B surface antigen (HBsAg) ni protini maalumu inayopatikana juu ya uso (surface) wa kuta za virusi vya homa ya ini B (Hepatitis B virus).
📌 𝗠𝗮𝗮𝗻𝗮 𝗵𝗮𝗹𝗶𝘀𝗶 𝘆𝗮 𝗵𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀 𝗯 𝘀𝘂𝗿𝗳𝗮𝗰𝗲 𝗮𝗻𝘁𝗶𝗴𝗲𝗻 (𝗛𝗕𝘀𝗔𝗴):
Ni alama ya kwanza ambayo huonekana kwenye damu baada ya mtu kuambukizwa virusi vya Hepatitis B (HBV).
Inapotokea kwenye kipimo cha damu, inaonyesha kwamba mtu ameambukizwa HBV na virusi bado vipo mwilini yani Positive.
👉🏿 Kipimo kina mistari miwili, mstari wa kwanza hufahamika kama Control Line ambao hubeba sample ya mgonjwa yani Damu.
👉🏿 Na mstari wa pili hufahamika kama Test line ambao huonyesha uwepo wa uso wa virus vya homa ya ini B.
Kipimo kinapo onyesha mistari miwili yenye rangi nyekundu huashilia kuwa mtu huyu bado yupo anaishi na maambukizi ya virus vya homa ya ini Hepatitis B Postive
- Ikitokea kipimo kimesoma mstari mmoja mwekundu huashilia mtu huyu tayari ameshapona maambukizi virus vya homa ya ini B ( negative )
🔎 𝗨𝗺𝘂𝗵𝗶𝗺𝘂 𝘄𝗮 𝗸𝗶𝗽𝗶𝗺𝗼 𝗰𝗵𝗮 𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀 𝗕 𝗦𝘂𝗿𝗳𝗮𝗰𝗲 𝗔𝗻𝘁𝗶𝗴𝗲𝗻 (𝗛𝗕𝘀𝗔𝗴)
Hizi ni baadhi ya umuhimu wa kipimo cha Hepatitis b surface antigen.
𝗞𝗶𝗽𝗶𝗺𝗼 𝗵𝗶𝗸𝗶 𝗸𝗶𝗻𝗮𝘀𝗮𝗶𝗱𝗶𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝘂𝘁𝗮𝗺𝗯𝘂𝘇𝗶 (𝗱𝗶𝗮𝗴𝗻𝗼𝘀𝗶𝘀):
Ikiwa 𝗛𝗕𝘀𝗔𝗴 𝗶𝗽𝗼 𝗽𝗼𝘀𝗶𝘁𝗶𝘃𝗲, inamaanisha mtu anaishi na maambukizi ya Hepatitis B (anaweza kuwa na maambukizi ya muda mfupi acute infection isiyo hitaji matibabu au yenye kuhitaji matibabu ya kuda mfupi sana na kupona kabisa au ya muda mrefu yenyw kuhitaji matibabu ili kuisaidia kinga kuweza kupambana na maambukizi na kurejesha seli za kinga zilizo chakaa au kufa, kuondoa seli za saratani ya ini na Cirrhosis.
Ikiwa 𝗛𝗕𝘀𝗔𝗴 𝗶𝗽𝗼 𝗻𝗲𝗴𝗮𝘁𝗶𝘃𝗲, mara nyingi inamaanisha hakuna virusi tena vya HBV kwenye damu mgonjwa anaweza kuwa amepona.
𝗕𝗮𝗮𝗱𝗵𝗶 𝘆𝗮 𝗗𝗮𝗹𝗶𝗹𝗶 𝘇𝗮 𝗺𝗮𝗮𝗺𝗯𝘂𝗸𝗶𝘇𝗶 𝘆𝗮 𝗛𝗕𝗩
Ikiwa antigen hii inabaki zaidi ya miezi 6 mfululizo, kawaida mtu huchukuliwa kuwa na Hepatitis B sugu (chronic infection).
- Ikiwa inatoweka ndani ya miezi michache, inaonyesha mwili umefanikiwa kupambana na virusi na mtu amepona.
𝗨𝗺𝘂𝗵𝗶𝗺𝘂 𝗸𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗮𝗺𝗯𝘂𝗸𝗶𝘇𝗶:
- Mtu akiwa na HBsAg positive na hajaanza matibabu yoyote ya kutibu na kudhibiti maambukizi, mgonjwa anaweza kueneza virusi kwa watu wengine kupitia damu, ngono, jasho au kutoka mama kwenda mtoto katika kipindi cha ujauzito, kujifungua au kunyonyesha.
➡️ 𝗞𝘄𝗮 𝗸𝗶𝗳𝘂𝗽𝗶: Hepatitis B surface antigen (HBsAg) = protini ya juu ya uso wa virusi vya HBV inayotumika kama kiashiria kikuu cha uwepo wa maambukizi ya Hepatitis B mwilini.
𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:- Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.
𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨.