Tafuta

Appointiment


*

Huduma ya Chanjo ya homa ya Ini kwa wagonjwa walio athirika na virus vya Hepatitis B (Virus vinavyo sababisha ugonjwa mkali wa ini na saratani)


Huduma ya chanjo hutolewa kwa watu wazima, watoto wadogo na vijana wasio kuwa na maambukizi ya virus vya homa ya ini (Hepatitis B)

𝗝𝗘 𝗡𝗜 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗠𝗔 𝗞𝗨𝗖𝗛𝗢𝗠𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗡𝗝𝗢 𝗡𝗜𝗞𝗜𝗪𝗔 𝗕𝗔𝗗𝗢 𝗡𝗔𝗜𝗦𝗛𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗠𝗕𝗨𝗞𝗜𝗭𝗜:


Hapana, si salama kuchoma chanjo ikiwa bado una maambukizi au dalili za ugonjwa. Hii ni kwa sababu:

 

𝗠𝘄𝗶𝗹𝗶 𝘂𝗻𝗮𝗵𝗶𝘁𝗮𝗷𝗶 𝗻𝗴𝘂𝘃𝘂 𝘇𝗮 𝗸𝘂𝗷𝗶𝗽𝗼𝗻𝘆𝗮:


  • Wakati una maambukizi, kinga ya mwili wako inafanya kazi kwa bidii kiasilia katika kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo.

     

  • Sasa kuchoma chanjo wakati huo huo kunaweza kuleta mzigo wa ziada kwa mfumo wa kinga, kudhoofisha zaidi uzalishwaji mnzuri wa seli hai za kinga, kusababisha mwili kuzalisha seli izo pasipo mpangilio, na kusababisha huchochezu uzalishwaji wa seli za kansa.

 

𝗞𝘂𝗼𝗻𝗴𝗲𝘇𝗮 𝗵𝗮𝘁𝗮𝗿𝗶 𝘆𝗮 𝗺𝗮𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝗻𝘆𝗲𝗺𝗲𝗹𝗲𝘇𝗶:

 

  • Kuchoma chanjo ukiwa na maambukizi kunaweza kuongeza hatari ya madhara ya chanjo, kama vile homa za mara kwa mara, maumivu ya mwili, uchovu usiyo isha, kuhusi kichefuchefu na kupoteza fahamu.

 

𝗖𝗵𝗮𝗻𝗷𝗼 𝗜𝗻𝗮𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗞𝘂𝘄𝗮 𝗜𝘀𝗶𝘆𝗼 𝗻𝗮 𝗨𝗳𝗮𝗻𝗶𝘀𝗶:


  • Mwili wako unaweza kushindwa kujenga kinga kamili kutokana na chanjo ikiwa unashughulika na maambukizi mengine.

 



𝗠𝗨𝗗𝗔 𝗚𝗔𝗡𝗜 𝗦𝗔𝗛𝗜𝗛𝗜 𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗖𝗛𝗢𝗠𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗡𝗝𝗢:


  • Muda sahihi wa kuchoma chanjo unategemea na aina ya chanjo, hali ya afya ya mtu, na ratiba inayopendekezwa na wataalamu wa afya kitaifa.

 

𝗨𝘁𝗮𝗿𝗮𝘁𝗶𝗯𝘂 𝘄𝗮 𝗸𝘂𝗰𝗵𝗼𝗺𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗷𝗼.

 

  • Tuna kushauri kuchoma chanjo baada ya kupona kabisa na kuwa katika hali nzuri ya afya.

     

  • Chanjo hutolewa kwa watu walio pona, hutolewa kwa watu walioko hatarini kuambukizwa na chanjo hii hutolewa kwa awamu tatu hadi kukamilisha, siku ya kwanza unapo chomwa, mwezi unaofuata na baada ya miezi sita ndipo unamalizia chanjo ya tatu.

 

𝗖𝗵𝗮𝗻𝗷𝗼 𝗸𝘄𝗮 𝘄𝗮𝘁𝗼𝘁𝗼 𝘄𝗮𝗱𝗼𝗴𝗼:

 

  • Watoto wachanga wanachanjwa mara tu wanapozaliwa au ndani ya wiki chache za maisha, kulingana na afya ya mama kama anaishi na magonjwa hatarishi ya kuambukiza pamoja na ratiba ya chanjo ya kitaifa.

     

  • Ratiba ya chanjo inajumuisha chanjo dhidi ya magonjwa kama polio, pepopunda, Hepatitis, surua, kifua kikuu (BCG), na nyinginezo.

 

𝗖𝗵𝗮𝗻𝗷𝗼 𝗸𝘄𝗮 𝘄𝗮𝘁𝘂 𝘄𝗮𝘇𝗶𝗺𝗮:

 

  • Chanjo kama vile tetanus (pepopunda) huchomwa kila baada ya miaka 10.

     

  • Chanjo kama ile ya homa ya manjano (Hepatitis) au HPV (Human Papiloma virus) zinaweza kuchomwa kulingana na umri wa mtu, matakwa yake, au hali fulani za kiafya kama vile mtu ametoka kupona kutoka katika hali ya kuishi na maambukizi.

 

𝗖𝗵𝗮𝗻𝗷𝗼 𝗽𝗶𝗮 𝗶𝗻𝗮𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗸𝘂𝗰𝗵𝗼𝗺𝘄𝗮 𝘄𝗮𝗸𝗮𝘁𝗶 𝘄𝗮 𝗱𝗵𝗮𝗿𝘂𝗿𝗮:

Wakati wa mlipuko wa magonjwa kama homa ya mafua au COVID-19, chanjo hutolewa kulingana na maelekezo ya wizara ya afya au WHO.


Ni muhimu kuchoma chanjo kwa muda uliopendekezwa ili kuongeza kinga ya mwili na kujilinda dhidi ya magonjwa sugu ya kuambukiza.

 

𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.


𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨.

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!