Visababishi na Madhara ya kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mlefu kwa mgonjwa wa homa ya ini
Choo kigumu au kukosa choo, ni tatizo la mtu au mgonjwa kukaa siku nyingi kama siku 2 tatu au hata wiki moja kupata choo au akipata choo basi choo iko kinakuwa kigumu (kuwa na wakati mgumu wa kutoa au kuanzisha kinyesi).
๐๐จ๐๐ข๐ฆ๐ ๐๐๐ข๐ข ๐๐ช๐ ๐ ๐จ๐๐ ๐ ๐๐๐๐จ, ๐๐จ๐ฃ๐๐ง๐ ๐๐๐ข๐ข ๐๐๐๐จ๐ ๐จ ๐๐ช๐ ๐ ๐๐ข๐ก๐๐ช๐ ๐ช๐ ๐๐ก๐:
Kukosa choo kwa muda mrefu na kupata choo kigumu (constipation) kwa mgonjwa wa ini ni hali inayoweza kuchangiwa na mambo kadhaa:
Baadhi ya Sababu zinazowezekana kama madhara yanayo sababishwa na hali ya kukosa choo kwa muda mlefu na kupata choo kigumu kwa mgonjwa wa ini :
๐ญ. ๐ ๐ฎ๐ฏ๐ฎ๐ฑ๐ถ๐น๐ถ๐ธ๐ผ ๐๐ฎ ๐ฐ๐ต๐ฎ๐ธ๐๐น๐ฎ ๐ธ๐๐ฎ ๐บ๐ด๐ผ๐ป๐ท๐๐ฎ ๐๐ฎ ๐ถ๐ป๐ถ
Wagonjwa wa ini mara nyingi hupunguza baadhi ya vyakula (mfano mafuta mengi, chumvi na sukari), na kama mgonjwa atakuwa mvivu wa kutumia mboga za majani kwa wingi na matunda ya kutosha huathiri kinyesi na mfumo mnzima wa mmengโenyo.
๐ฎ. ๐ ๐ฎ๐ฑ๐ต๐ฎ๐ฟ๐ฎ ๐๐ฎ ๐๐ฎ๐๐ฎ ๐ธ๐ฎ๐บ๐ฎ ๐๐ถ๐น๐ฒ ๐ฃ๐ฎ๐ฟ๐ฎ๐ฐ๐ฒ๐๐ฎ๐บ๐ผ๐น ๐ฎ๐ ๐ง๐ฒ๐ป๐ผ๐ณ๐ผ๐๐ถ๐ฟ:
Baadhi ya dawa za kupunguza maumivu na kufubaza virus kwa matatizo ya ini au maumivu (mfano dawa zenye madini chuma/iron, dawa za maumivu) husababisha choo kigumu.
๐ฏ. ๐จ๐ฝ๐๐ป๐ด๐๐ณ๐ ๐๐ฎ ๐บ๐ฎ๐ท๐ถ ๐บ๐๐ถ๐น๐ถ๐ป๐ถ
Mgonjwa wa ini anaweza kuwekewa kizuizi cha kunywa maji mengi kutokana na uvimbe wa tumbo (ascites), hali hii huleta choo kigumu.
๐ฐ. ๐๐๐ฝ๐๐ป๐ด๐๐ฎ ๐ธ๐๐ฎ ๐๐ต๐๐ด๐ต๐๐น๐ถ ๐๐ฎ ๐ถ๐ป๐ถ ๐๐ฎ๐ป๐ถ ๐น๐ถ๐๐ฒ๐ฟ ๐บ๐ฒ๐๐ฎ๐ฏ๐ผ๐น๐ถ๐๐บ ๐ธ๐๐ฒ๐ป๐๐ฒ ๐๐ฝ๐ฎ๐ป๐ฑ๐ฒ ๐๐ฎ ๐ฒ๐ป๐๐๐บ๐ฒ๐ ๐๐ถ๐บ๐ฒ๐ป๐ดโ๐ฒ๐ป๐๐ฎ.
Wagonjwa wengi hasa wenye tatizo hili kwa miaka mingi, huanza kupata magonjwa ya tumbo kama vile tumbo kujaa gesi na kuhisi hali ya kushiba shiba muda wote, hupelekea mgonjwa wa ink kupumzika sana, hivyo matumbo husogea taratibu.
๐ฑ. ๐๐๐ต๐ฎ๐ฟ๐ถ ๐๐ฎ ๐๐ด๐ผ๐ป๐ท๐๐ฎ ๐๐ฒ๐ป๐๐ฒ๐๐ฒ:
Ini likiwa na shida, mfumo wa mmengโenyo na homoni zinazosaidia usafishaji wa chakula zinaweza kuathirika.
๐ ๐ฎ๐ฑ๐ต๐ฎ๐ฟ๐ฎ ๐๐ฎ ๐ธ๐๐ฒ๐ป๐ฑ๐ฒ๐น๐ฒ๐ฎ ๐ธ๐๐๐ฎ ๐ป๐ฎ ๐ฐ๐ต๐ผ๐ผ ๐ธ๐ถ๐ด๐๐บ๐ ๐ธ๐๐ฎ ๐บ๐ด๐ผ๐ป๐ท๐๐ฎ ๐๐ฎ ๐ถ๐ป๐ถ:
Inaongeza shinikizo tumboni, hali inayoweza kuchochea maumivu ya upande wa kulia.
Inaweza kuchochea encephalopathy ya ini (sumu ya ammonia kuongezeka mwilini) kwa sababu taka hazitoki vizuri.
- Huchangia vidonda au kupata bawasiri.
๐ ๐ถ๐ธ๐ฎ๐ธ๐ฎ๐๐ถ ๐๐ฎ ๐ธ๐๐๐ฎ๐ถ๐ฑ๐ถ๐ฎ ๐ธ๐๐ฝ๐๐ป๐ด๐๐๐ฎ ๐ต๐ฎ๐น๐ถ ๐ต๐ถ๐๐ถ ๐ป๐ฎ ๐ธ๐๐๐ถ๐ฏ๐:
Kama ni mgonjwa wa inj, fikia huduma za matibabu ya homa ya ini.
Kula mboga za majani na matunda yenye nyuzi (fiber) laini kama papai, parachichi, ndizi zilizoiva, boga.
Kutumia nafaka zisizokobolewa (uji wa shayiri, nafaka nzima).
Kunywa maji kwa kiwango kinachoruhusiwa na daktari wako (kwa kuwa wagonjwa wa ini wengine wana kizuizi cha maji).
Kutembea au kufanya mazoezi mepesi kadri ya uwezo.
- Kuuliza kwa daktari kuhusu dawa za kusaidia kulainisha choo (laxatives salama kwa wagonjwa wa ini, kama lactulose).
๐ ๐ฃ๐๐ก๐๐ข ๐ ๐๐๐๐จ๐ ๐ช๐ ๐ฉ๐๐ก๐ฌ๐ช๐๐๐ ๐ก๐ ๐๐๐ฆ๐๐ ๐ฉ๐๐ก๐๐ฉ๐ฌ๐ข๐ช๐๐ญ๐ ๐๐จ๐ฆ๐๐๐๐๐ ๐๐จ๐ฃ๐จ๐ก๐๐จ๐ญ๐ ๐๐๐๐ ๐ฌ๐ ๐๐จ๐ฃ๐๐ง๐ ๐๐๐ข๐ข ๐๐๐๐จ๐ ๐จ ๐๐จ ๐๐จ๐๐ข๐ฆ๐ ๐๐๐ข๐ข ๐๐ช๐ ๐ ๐๐ข๐ก๐๐ช๐ ๐ช๐ ๐๐ข๐ ๐ ๐ฌ๐ ๐๐ก๐:
Hapa kuna mpango maalum wa vyakula na vinywaji vinavyoweza kusaidia mgonjwa wa ini kupunguza tatizo la choo kigumu, ukiwa umezingatia kwamba wagonjwa wa ini mara nyingi wanahitaji ulaji bora na usio mzito kwa ini:
๐ ๐๐ข ๐ ๐ก๐ญ๐จ๐ฅ๐ ๐ช๐ ๐๐ฆ๐จ๐๐จ๐ ๐๐ช๐ ๐ ๐๐ข๐ก๐๐ช๐ ๐ช๐ ๐๐ก๐:
Uji wa shayiri (oats) au ulezi, bila sukari nyingi.
Parachichi lililoiva au kipande kimoja cha ndizi iliyoiva (kwa umuhimu wa kupata nyuzi nyuzi na madini ya potasiamu).
- Kikombe cha chai ya kienyeji (kama mchaichai au tangawizi kidogo โ ikiwa haileti kiungulia).
๐ ๐๐ข ๐ ๐ก๐ญ๐จ๐ฅ๐ ๐ช๐ ๐ ๐๐๐๐ก๐ ๐๐ช๐ ๐ ๐๐ข๐ก๐๐ช๐ ๐ช๐ ๐๐ก๐:
Wali wa kahawia (brown rice) au ugali wa dona (una nyuzi nyingi).
Mboga za majani zilizopikwa kwa mvuke au kuchemshwa: matembele, mchicha, spinach, brokoli.
Maharage mekundu/soya/lentils (chanzo cha protini na nyuzi).
- Kipande kidogo cha samaki wa kuchemsha au kuoka.
๐ ๐ฉ๐๐ง๐๐๐จ๐ก๐ช๐ (๐ฆ๐ป๐ฎ๐ฐ๐ธ๐)
Papai lililoiva (linasaidia sana kulainisha choo).
Embe au matunda yenye nyuzi laini.
- Karanga au lozi kwa kiasi kidogo (healthy fats na fiber).
๐ ๐๐ข ๐ ๐ก๐ญ๐จ๐ฅ๐ ๐ช๐ ๐๐๐ข๐ก๐ ๐๐ช๐ ๐ ๐๐ข๐ก๐๐ช๐ ๐ช๐ ๐๐ก๐:
Viazi vitamu vilivyochemshwa/kuokwa.
Mboga za kuchemshwa: kabichi, sukuma wiki, bamia (bamia husaidia kulainisha choo).
- Supu nyepesi ya mboga au dengu.
๐ฉ๐๐ก๐ฌ๐ช๐๐๐ ๐ฅ๐๐๐๐๐ ๐๐ช๐ ๐๐๐ฌ๐ ๐ฌ๐ ๐๐ก๐ ๐ก๐ ๐ ๐๐จ๐ ๐ข ๐ช๐ ๐๐๐๐๐จ๐๐:
Maji safi na salama kulingana na kiwango kilichoelekezwa na daktari (kawaida wagonjwa wa ini wenye uvimbe hupangiwa kikomo cha maji, mfano si zaidi ya lita 1โ1.5 kwa siku).
Juisi asilia isiyo na sukari nyingi, mfano juisi ya papai, juisi ya tikiti maji kwa kiasi.
- Epuka soda, vinywaji vyenye kafeini nyingi, na vileo kabisa.
๐๐๐๐๐๐ ๐ฌ๐ ๐ฉ๐ฌ๐๐๐จ๐๐ ๐ฉ๐ฌ๐ ๐๐จ๐๐ฃ๐จ๐๐ช๐ ๐๐ช๐ ๐ ๐๐ข๐ก๐๐ช๐ ๐ช๐ ๐๐ก๐:
Vyakula vya kukaanga na mafuta mengi, kama Sambusa, Vitumbua, Keki, maandazi, samaki na kuku wa kukaanga pamoja na chips.
Nyama nyekundu nzito (inaweza kumchosha mgonjwa wa ini).
Sukari nyingi na vyakula vilivyosindikwa.
Chakula chenye pilipili nyingi au viungo vizito (huchochea asidi).
- Ndizi mbichi na ndizi ngumu (zinaweza kufanya choo kigumu zaidi).
๐ง๐จ๐ ๐๐ ๐ฉ๐๐๐ข๐๐๐ญ๐ข ๐๐๐ฉ๐ ๐ฉ๐ฌ๐ ๐ญ๐๐๐๐:
Tumia lactulose ikiwa daktari ameagiza โ husaidia kulainisha choo na kupunguza sumu ya ammonia.
Kuwa na ratiba ya kula mara ndogo ndogo (mil 4โ5 kwa siku badala ya mil 2 mikubwa).
- Kutembea taratibu kila siku (hata dakika 15) kunasaidia harakati za utumbo.
๐๐จ๐ ๐๐จ๐๐:- Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.
๐๐ฎ๐ฟ๐ถ๐ฏ๐ ๐๐๐ธ๐๐ต๐๐ฑ๐๐บ๐ถ๐ฒ ๐ธ๐๐ฎ ๐ฐ๐ต๐ฎ๐ป๐ด๐ฎ๐บ๐ผ๐๐ผ ๐๐ฎ ๐ฎ๐ณ๐๐ฎ ๐๐๐ป๐ฎ๐๐ผ๐ฎ ๐ต๐๐ฑ๐๐บ๐ฎ ๐๐ฎ ๐ฉ๐๐ฃ๐๐ ๐ข, ๐จ๐ฆ๐๐๐จ๐ฅ๐ ๐ก๐ ๐ ๐๐ง๐๐๐๐๐จ.