Tafuta

Appointiment


*

Kipimo cha homa ya ini [Hepatitis B surface Antigen]


Pima homa ya ini, tambua afya yako, anza matibabu, Pona kisha choma chanjo

𝗛𝗘𝗣𝗔𝗧𝗜𝗧𝗜𝗦 𝗕 𝗦𝗨𝗥𝗙𝗔𝗖𝗘 𝗔𝗡𝗧𝗜𝗚𝗘𝗡 (𝗛𝗕𝘀𝗔𝗴)

𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀 𝗕 𝘀𝘂𝗿𝗳𝗮𝗰𝗲 𝗮𝗻𝘁𝗶𝗴𝗲𝗻 (𝗛𝗕𝘀𝗔𝗴) ni protini maalum inayopatikana kwenye gamba la virusi vya Hepatitis B. 

Kipimo hiki hutumika kuangalia kama mtu ana maambukizi ya Hepatitis B kwa sasa.


1️⃣ 𝗛𝗕𝘀𝗔𝗴 𝗶𝗸𝗶𝘄𝗮 𝗽𝗼𝘀𝗶𝘁𝗶𝘃𝗲 (𝗶𝗺𝗲𝗼𝗻𝗲𝗸𝗮𝗻𝗮 𝗺𝗶𝘀𝘁𝗮𝗿𝗶 𝗺𝗶𝘄𝗶𝗹𝗶)

✔️ Ina maana virusi vya Hepatitis B vipo mwilini.


𝗠𝘁𝘂 𝗮𝗻𝗮𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗸𝘂𝘄𝗮:

✔️ Ameambukizwa hivi karibuni (acute infection) isiyo hitaji matibabu na mtu anaweza kupona bila hata dawa au


✔️ Ana maambukizi ya muda mrefu (yenye kuhitaji matibabu zaidi).


2️⃣ 𝗛𝗕𝘀𝗔𝗴 𝗶𝗸𝗶𝘄𝗮 𝗻𝗲𝗴𝗮𝘁𝗶𝘃𝗲 (𝗵𝘂𝗼𝗻𝗲𝗸𝗮𝗻𝗮 𝗺𝘀𝘁𝗮𝗿𝗶 𝗺𝗺𝗼𝗷𝗮)

✔️ Mara nyingi ina maana mtu hana maambukizi ya Hepatitis B kwa sasa.


✔️ Anaweza kuwa amepona kutoka katika kuishi na maambukizi ya virus vya Hepatitis B au hajawai kuambukizwa


💊 𝗠𝗮𝗱𝗮𝗸𝘁𝗮𝗿𝗶 𝗺𝗮𝗿𝗮 𝗻𝘆𝗶𝗻𝗴𝗶 𝗵𝘂𝗮𝗻𝗴𝗮𝗹𝗶𝗮 𝗽𝗮𝗺𝗼𝗷𝗮 𝗻𝗮 𝘃𝗶𝗽𝗶𝗺𝗼 𝘃𝗶𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲 𝗸𝗮𝗺𝗮:

1️⃣ 𝗛𝗕𝗩 𝗗𝗡𝗔 → kuangalia kiwango cha virusi


2️⃣ 𝗛𝗕𝗲𝗔𝗴 → kuona kasi ya uzalishaji wa virusi


3️⃣ 𝗔𝗻𝘁𝗶-𝗛𝗕𝘀 → kuangalia kinga dhidi ya Hepatitis B


4️⃣ 𝗟𝗶𝘃𝗲𝗿 𝗳𝘂𝗻𝗰𝘁𝗶𝗼𝗻 𝗧𝗲𝘀𝘁 (𝗔𝗟𝗧/𝗔𝗦𝗧) → Kuangalia utendaji kazi wa ini na vimeng'enya.


𝗠𝗔𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗕𝗜𝗟𝗔 𝗛𝗢𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜, 𝗜𝗡𝗔𝗪𝗘𝗭𝗘𝗞𝗔𝗡𝗔

𝗧𝗶𝗯𝘂 𝗜𝗡𝗜 - 𝗢𝗸𝗼𝗮 𝗠𝗮𝗶𝘀𝗵𝗮

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!